Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amempongeza Donald Trump kwa kuchaguliwa kuongoza taifa la Marekani katika uchaguzi uliofanyika jana Novemba 5,2024.
Kupitia ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa X, Rais Samia ameandika: “Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Donald Trump, Rais mteule wa Marekani, kwa ushindi wako katika uchaguzi. Nakutakia heri na mafanikio."
Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa anatarajia kushirikiana na Trump kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED