Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Sharifa Suleiman, leo amechukua fomu kuwania nafasi ya uenyekiti wa baraza hilo.
Kwa takriban miaka minne, Sharifa amekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, nafasi aliyoichukua wakati chama hicho kilipokumbwa na migogoro mbalimbali, ikiwemo kuvuliwa uanachama kwa baadhi ya viongozi.
Katika kipindi chake cha uongozi, kipaumbele chake kikubwa kilikuwa kuwaunganisha wanawake ndani ya chama.
“Baada ya kukaimu kwa miaka minne, sasa nachukua fomu kuwania nafasi ya uenyekiti nikiwa na lengo la kuwaunganisha wanawake kwa ujumla na kufanya harakati za kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, sambamba na kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa CCM,” amesema Sharifa.
Sharifa ameahidi kuimarisha ushirikiano kati ya wanawake na CHADEMA ili kuhakikisha chama kinaendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika mchakato wa kuleta mabadiliko nchini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED