Serikali imeandaa mafunzo maalum kwa watu wanaoenda kufanya kazi nje ya nchi ili waweze kuendana na Soko la ajira nje ya mipaka ya Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ajira kutoka Ofisi ya Waziri ya Mkuu ,Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Joseph Nganga, aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Ridhiwani Kikwete.
Akizungumza kwenye Mkutano maalum wa kujadili kuhusu Uhamiaji wa Wafanyakazi unaolenga kukuza ajira salama zenye staha kwa wahamiaji wa Kitanzania na kupunguza vihatarishi mbalimbali alisema, Watanzania wanatakiwa kuwa na uelewa juu ya maswala yanahusiana na ajira za nje ya nchi.
Aidha ametoa wito kwa Watanzania wanaoenda kufanya kaz nje ya nchi waweze kutumia mawakala wanaotambulika Seeikalini ili kuepuka changamoto zinazoweza kutoa kwani inaweza kuwa rahisi kupata msaada na kudhaminika unapopata shida katila kazi zako ukiwa nje ya nchi.
'Ni mhimu kuwa na ujuzi maalum unaohusiana na ajira za nje ya nchi ili kuweza kuleta Maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla" aliseama Nganga.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Diaspora ambao ni watanzania wanaoishi Ughaibuni, Sylivester Mbili, amesema watanzania wanaoishi nje ya Nchi wajitahidi kufuta taratibu za kuishi ugenini ili waweze kusaidika pale wanapopata changamoto yoyote hasa zinazohusina na maswala mazima ya ajira.
Amesema swala la ajira salama ni mhimu kuzingatiwa kwani itasaidia kuondoa hali ya sintofahamu inapotokea hali changamoto katika ajira ya Watanzania wanakaa nje ya nchi na hasa unapofuata utaratibu uliokidhi vigezo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED