WIZARA ya Fedha, imesema kuna aina sita za kustaafu ambazo zote zinapaswa kuandaliwa mara mwajiriwa anaposaini mkataba wa kazi au kuanza kazi kwenye sekta binafsi.
WIZARA ya Fedha, imesema kuna aina sita za kustaafu ambazo zote zinapaswa kuandaliwa mara mwajiriwa anaposaini mkataba wa kazi au kuanza kazi kwenye sekta binafsi.
Akizungunza na wahariri wa vyombo mbalimbali, Ofisa Mwandamizi Kitengo cha Pensheni wa Wizara ya Fedha, Ushindi Kalinga, amesema wananchi wengi wanajua kustaafu kunaanza mara baada ya kufikisha umri wa miaka 60 kwa mujibu wa sheria au kwa hiyari ukiwa na miaka 55 bila kujua kuna aina nyingine za kustaafu.
Amezitaja kuwa ni kustaafu jwasababu za ugonjwa ambazo haziangalii imri,kustaafushwa ikiwa ofisi itafutwa kama ilivyokuwa waliokuwq wafanyakazi wa Jumumuiya ya Afrika Mashariki ilivyovunjwa,serikali inaweza kukustaafisha kwa manufaa ya umma,na kustaafu kwa sababu ya kifo.
"Tuondoke kwenye dhana ya kwamba kustaafu ni lazima kufikisha umri,muhimu kutengeneza utaratibu utakaotusaidia kipindi hatuna nguvu,"amesema.
Aidha,amesema ni muhimu kila mmoja kuwa na utaratibu wa kuweka akiba yake,kwani uzoefu unaonyesha watu wanapostaafu wanaingia kwenye changamoto za kimaisha kwakuwa wengi wanapokuwa kazini hawaangalii kesho yao itakuwaje.
Aidha,amesema watu wengi wanapokuwa na nguvu wanafikiri kustaafu hakutatokea,lakini wanapaswa kujua kunaanza mara baada ya kusaini mkataba wa kazi.
"Wakati ukiwa ofisini wafanyakazi wenzako wamekuzunguka unaona ni maisha mazuri,ila kuna wakati utakuwa mwenyewe,hivyo lazima ujiwekee utaratibu wa maisha yako ya baadaye,"amesema Kalinga.
Amesema iwapo familia ina mtu alikuwa mfanyakazi akafariki atakuwa na mafao yake hivyo familia zinapaswa kujua njia sahihi kama ni wizarani au kwenye mifuko ya kihadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED