MWISHO wa mwezi uliopita, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametua nchini Marekani kwa ziara inayohusu usalama wa chakula na akakutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Millenium Challenge Corporation (MCC), mwanamama mwenzake, Alice Albright.
Ni mazungumzo yaliyojikita kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya pande hizo mbili mnamo tarehe 30 mwezi uliopita, Tanzania ni kati ya mataifa wabia wa asasi hiyo yenye makao makuu nchini Marekani.
Nchi zingine za Afrika wabia wa MCC ni kama : Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Morocco, Msumbiji, Namibia, Niger, Tunisia na Zambia.
Pia, kuna mataifa wadau kama, Ethiopia, Gambia, Kenya, Liberia, Rwanda na Uganda.
Asasi hiyo ina miaka 20 tangu kuanzishwa, mwasisi wake ni Rais George Bush, ikiwa na makao makuu Marekani na majukumu yake ni kukuza uchumi, kufungua milango ya masoko kwa nchi husika na viwango vya maisha ya wakazi wake.
Ubia wa MCC na nchi zinazochaguliwa unajumuisha pale inaporidhishwa na sera husika, pia kasi yake katika ukuaji uchumi kwa mujibu wa taratibu zake, mhitaji huomba mkopo mahsusi pale mradi anaonadi unapopitishwa.
Rais Dk. Samia amekutana na mkuu huyo wa MCC, huku imepita miezi minane tangu Februari mwaka huu, Naibu Mtendaji Mkuu wa asasi hiyo ya MCC, Chidi Blyden, alipokuwa nchini kukagua maendeleo ya miradi wanayosimamia, sambamba na mipango yao na serikali.
Muda mfupi kabla ya kuondoka nchini alikokutana na viongozi wa kiserikali akiwamo Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Blyden akaitaja Tanzania kuwa mbia wao muhimu, akiwa na kauli:
“Tunatarajia juhudi zetu za pamoja kuimarisha utawala bora kwa upana na ulio endelevu katika maendeleo ya kiuchumi.”
Ndani ya ziara hiyo nchini, akakagua miradi ya MCC ya mabadiliko, akiwaelimisha vijana kuhamia maisha ya digitali na fursa za kisera nchini, kwenye mabadiliko kisera yaliyoko kitaifa na kimataifa.
MJADALA WA CHAKULA
Akiwa nchini Marekani wiki iliyopita, Dk. Samia akashiriki mjadala maalum wa usalama wa chakula, akiwa kati ya wakuu wa nchi wanne wa Kiafrika waliokaribishwa, wenzake wanatoka Sierra Leone, Madagascar na Nigeria, akafafanua azma ya kuifanya taifa lake ngome ya upatikanaji chakula.
Rais Dk. Samia, akaeleza mikakati ya serikali kuibua mabadiliko makubwa ya kilimo, ikilenga Tanzania kujitosheleza na kuwa ngome ya chakula, njia za kupitia anataja malengo matatu ya msingi, nchi imwejiwekea.
Hayo ni kwa mujibu malekezo yanayorejewa, kwa hatua taifa imezichukua katika kikao kinachohusu chakula, kilichofanyika Dakar, Senegal, Januari mwaka jana.
Sura ya kwanza, anaitaja ni kuifanya Tanzania ipate tija katika kilimo, kuanzia wingi wa bidhaa, hadi ubora wake, iwe inafikika na gharama nafuu.
Aidha, lingine linagusa maboresho katika hifadhi ya chakula hicho kikishavunwa shambani kupunguza kinachopotea katika uzalishaji, akiwa na ufafanuzi kwamba kipaumbele ni kuongezea thamani mazao ya kilimo.
Kwa mujibu Rais Dk. Samia, ni hali itakayoisaidia nchi kuhimili upatikanaji mazao ya chakula na manufaa ya kiuchumi kwa wakulima wa Kitanzania.
Mtazamo huo wa kufanya mageuzi wa uzalishaji hadi kuhudumia bidhaa hiyo, ulionekana kuwagusa wadau wa Kimarekani, katika mjadala huo hata kuvuta tabasamu lao.
Dira ya tatu ya Rais Dk. Samia, inagusa ubunifu wa kuwa na ghala la chakula ikiwa na mitazamo mipana kugusa maslahi yanayovuka mipaka, akieleza matarajio kwamba dira tajwa itafikiwa.
“Hatujafikia malengo, lakini ninachokuhakikishia tuko njiani,” anasema Dk. Samia, akieleza serikali imebuni Baraza la Ushauri wa Chakula, lililoundwa kwa mujibu wa maelekezo ya kikao cha maendeleo ya uchumi cha wakuu wa nchi, waliokutana na wataalamu, pia asasi binafsi, huko Senegal.
Jukumu kuu la chombo hicho analitaja ni kuhakikisha hatua inapigwa katika kilimo cha chakula nchini. Rais akiwa na ufafanuzi: “Inafanya kazi nzuri katika kuishauri serikali namna ya kutekeleza kuhusu upatikanaji chakula na usalama wake.”
Dk. Samia anasema, dhima ya chombo hicho cha ushauri ni kuhakikisha Watanzania wanapata chakula cha kutosha, salama na chenye viini lishe muhimu.
Katika mjadala huo wa wiki iliyopita ambao Dk.Samia alikuwa mgeni mwalikwa, m[po1] waka huu mada yake imegusa “umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi, pia kuboresha kilimo barani Afrika.’
Tanzania kwa namna yake, inatajwa kuwa na faida ya ziada katika ardhi yenye rutuba na wajuzi wa kazi za shamba, wanaotajwa kuwa vivutio kwa wawekezaji wa sekta hiyo.
Pia, Dk. Samia, akawa na fursa ya mjadala wa faragha na maofisa wa serikali, pia taasisi binafsi za Marekani akinadi fursa za kilimo nchini Tanzania, hadi mnyororo mzima wa thamani wa kilimo uliopo nchini.
Rais akawasisitizia haja ya kushirikiana nao, hata Tanzania ichukue nafasi kimataifa kuwa mstari wa mbele katika kukabili njaa na utapiamlo duniani.
KIKAO CHA DAKAR
Ni mkutano uliofanyika mwezi Januari mwaka jana, jijini Dakar, Senegal ukiwakusanya wakuu wa nchi mbalimbali kuwataka waandae rasilimali zao na wadau wa maendeleo kuwekeza katika sekta kilimo kuzalisha chakula.
Hiyo inaendana na kuondoa vizingiti vyote katika maendeleo ya kilimo, ikisaidiwa na miradi mipya barani Afrika iongezeke kila mwaka kwa kiwango Dola za Marekani Trilioni moja, ifikapo mwaka 2030.
Hapo inajumuoshja mitazamo inayogusa maboresho ya miundombinu, mifumo ya hali ya hewa, ikiwamo mitaji binfasi inayowaunga mkono kuongeza thamani ya chakula n ahata kuongeza kapu la chakula.
Tafsiri pana inayojengwa hapo ni kuanzia wawekezaji wanaotimiza makubaliano yao na serikali, wakizama katika mfumo wa ubia wa kuzalisha chakula, wakishirikiana na wakuu wa kibenki na wizara zenye dhamana za kilimo, wadau binafsi na taasisi za kifedha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED