WIKI YA MAJI; DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI

By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili
Published at 03:39 PM Mar 23 2025
DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI
Picha: Mpigapicha Wetu
DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI

WIZARA ya Maji, imeikabidhi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), hundi la shilingi milioni 20, kwa ajili ya matibabu kwa watoto wenye changamoto mbalimbali za magonjwa ya moyo.

Hundi ya fedha hizo, imekabidhiwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara hiyo, Mhandisi Mwajuma Waziri, kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Angela Muhozya. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi hundi hiyo, Katibu Mkuu Mwajuma, amesema ziara hiyo ni sehemu ya shamrashamra za wiki ya maji, inayofanyika kila mwezi wa tatu kila mwaka 

“Sisi tunatambua ukubwa wa tatizo la moyo, kwa sababu hata sisi hivi karibuni tulimpoteza mfanyakazi mwenzetu ambaye alifariki ghafla mkoani Dodoma, kwa hiyo tukisikia mtu ana changamoto ya moyo tunapata hisia kuhusu tatizo hilo,” amesema.

72ead825-ca3b-4c3d-8631-df0fae6c19b7.jpg 339.56 KB
Pia amesema Wizara ya Maji, imeandaa utaratibu, wafanyakazi wake watakuwa wakifika kwenye taasisi hiyo, kwa ajili ya kufanya vipimo, ili watakaobainika kuwa na tatizo watibiwe mapema. 

Amesema waliamua kuweka utaratibu huo wa kupima afya mara kwa mara, baada ya kubaini kuwa kuna watumishi wengi wanaosumbuliwa na moyo ambao wakipima mapema watatibiwa na kuokoa maisha. 

Amesema Wizara ya Maji, kupitia taasisi zake itaendelea kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia watoto na watu wazima wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo maeneo mbalimbali nchini. 

DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI
“Nimeambiwa kwamba mnapanga kuongeza idadi ya wataalamu wa moyo, hilo ni jambo jema sana kwa sababu ongezeko hilo litakuwa msaada mkubwa kwasababu watu wenye matatizo watatibiwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa,” amesema. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Angela Muhozya, ameshukuru wizara hiyo, kwa msaada huo na kuomba wadau wengine waige mfano huo kwani wahitaji wa matibabu ya moyo wako wengi. 

Amesema huduma za moyo bado hazijafika kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuongeza kuwa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo wamekuwa wakigundulika wakiwa wamechelewa. 

“Ndiyo maana tumeanzisha huduma ya kwenda mikoa mbalimbali kila mwezi, kutoa huduma za upimaji na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya mikoani ili waweze kugundua tatizo mapema, ili wawahishwe JKCI watibiwe haraka,” amesema. 

Aidha, amesema wagonjwa wengi wanaowachukua kutoka mikoani wanakuwa wanahitaji huduma ya kibingwa ya upasuaji wa tundu dogo na tiba gharama yake iko juu kutokana na vifaa vinavyotumika kwenye matibabu hayo na dawa. 

“Matibabu ni gharama kubwa kwa hiyo tukipata wadau wakutusaidia kama nyinyi tunafurahi sana kwasababu wagonjwa wengi wanatoka familia za kipato cha chini sana kwa hiyo wakipata matibabu mapema wanakwenda kuendelea na kazi zao kama kawaida za kuzalisha uchumi,” amesema. 

DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI
Bingwa wa Magonjwa ya mMoyo JKCI, Dk. Stella Mongella, amesema idadi kubwa ya watoto wanazaliwa wakiwa na shida kwenye moyo yakiwemo ya kuzaliwa nayo kama matundu, mishipa kubana na mishipa kuvurugika. 

Amesema maradhi hayo yanaweza kumpata mtoto aliyetumboni kama mama mjamzito atapata shinikizo la damu na sukari kuwa nyingi pamoja na maambukizi mengine ya virusi mbalimbali. 

“Zaidi ya matatizo ya kuzaliwa nayo mtoto anaweza kupata maradhi haya ukubwani kama moyo kuwa mkubwa na dalili ya mtoto mwenye shida ya moyo ni kama kukua kwa shida, kupumua kwa shida na kutoka jasho jingi na katika kliniki yetu hapa tunapata watoto 10 kila siku wenye shida ya moyo,” alisema.Alisema watoto wanaohitaji matibabu ya moyo ya upasuaji wa kufungua kifua au kupitia mishipa ni 500 kila mwaka na kwamba idadi imekuwa ikiongezeka kila mwaka na gharama zake ni kubwa kutokana na vifaa na dawa zinazotumika. 

DAWASA yakaibidhi hundi ya milioni 20 JKCI
Meneja Mkuu wa Global Medicare, Daniel Lazaro, amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara, kwa kuwa walipoambiwa wachangie matibabu ya watoto wenye changamoto ya moyo, walitoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha wanatoa mchango wao. 

“Kwa taarifa iliyotolewa na daktari bingwa, inaonyesha tatizo bado ni kubwa na safari bado ni ndefu sana kwa hiyo tunaomba tutakapokuja tena mtuunge mkono kwasababu huduma hizi za upasuaji ni endelevu na tunatamani kumaliza wote wenye changamoto ya moyo,” amesema. 

Mwakilishi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,  Evarlasting Lyaro, amesema huo ni mwanzo tu wa ushirikiano na JKCI na kwamba wataandaa makubaliano ‘MoU; kwa ajili ya kushirikiana kupima afya za wafanyakazi.