NAIBU Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, leo ameomba msamahama ikiwa ni siku mbili kabla ya kujitetea kwa saa mbili (dakika 120) mbele ya umma juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi.
Leo Oktoba 6,2024, Gachagua aliomba radhi wakati wa ibada wakati wa Ibada wa Kitaifa ya Maombi jijini Nairobi, na kusema kama kuna aliyemkosea akiwa Naibu rais, amsamehe kutoka moyoni.
Pia alimuomba msamaha Rais William Ruto, wabunge waliowasilisha hoja katika Bunge la Taifa ya kumwondoa madarakani , na Wakenya kwa makosa aliyoyafanya.
“Ningependa kumwambia kaka yangu Rais William Ruto, kama katika juhudi zetu za kufanyakazi, nimemkosea, tafadahli anisaidie kwa moyo wake kunisamehe. Ikiwa mke wangu na mtoto wangu katika majukumu yao wamemkosea basi awasamehe pia,”amesema
Bunge la Taifa lilianza mchakato wa kumshtaki na kumng’oa madarakani Naibu Rais, baada ya Spika Moses Wateng’ula kuzikubali hoja 11 zilizowasilishwa na Mbunge wa Kibwezi West, Mwengi Mutuse.
Aidha, jumla ya wabunge 291 kati ya 249 wa Bunge la Taifa wamesaini hoja ya kumshataki na kumng’oa madarakani Naibu huyo.
Ibara ya 150 ya Katiba ya Kenya inaeleza masharti ya kuondolewa kwa Naibu Rais, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa sheria na kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake.
Aidha, hoja ya kumshtaki lazima iungwe mkono na angalau theluthi moja ya wabunge 117 katika Bunge ili taratibu zianze ikiwa Bunge la Kitaifa na Seneti wataridhia kwa theluthi mbili.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED