Mgombea Urais kupitia Chama cha Allience For Africa Farmers Party(AAFP) , Kunje Ngombale Mwiru' amewashukuru wanachama na wajumbe wa chama hicho kwa kumchagua kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu huku akitaka amani itawale.
Shukrani hizo amezitoa leo Mei 4, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari mbali na kuwashukuru wajumbe na wanachama ameishukuru pia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwa kusimamia zoezi la kupitisha mgombea. Katika mkutano mkuu maalum wa chama uliofanyika April 29, 2025 Temeke Jijini Dar es Salaam.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED