Msigwa asikitishwa maofisa habari wa serikali kuwa wabeba mikoba ya viongozi

By Paul Mabeja , Nipashe Jumapili
Published at 02:19 PM May 25 2025
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
PICHA: PAUL MABEJA
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameeleza kusikitishwa na tabia ya maofisa habari wa serikali kuacha majukumu yao ya kuisemea na kuwa wabeba mikoba ya viongozi.

Msigwa, amesema hayo Mei 24, jijini Dodoma, wakati akifunga kikao kazi kwa maofisa habari wa serikali wa mikoa, wilaya na taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 
Amesema, maofisa habari wengi wameacha majukumu yao ya msingi ya kuisemea na kuitetea pale ambapo kumekuwepo na taarifa mbalimbali za upotoshaji ambazo zimekuwa zikichapishwa na watu wenye nia ovu ya kuichafua serikali.
 
“Maofisa habari wengi hawatekelezi wajibu wao wa kuisemea serikali na kutetea pale ambapo kumekuwepo na taarifa za upotoshaji zinazaoichonganisha serikali na wananchi wake.
 
“Maofisa habari wengi wamekuwa hawafanyi wajibu wao bali wamekuwa wabeba mikoba ya viongozi, jambo ambalo siyo jukumu waliloajiriwa nalo hivyo ipo haja ya kubadilika na kuanaza kutekeleza wajibu wao wa kuisemea serikali katika mambo mazuri ambayo