MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema bado hajaona dalili za wananchi kutokukiamini chama hicho kutokana na kazi iliyofanywa na chama hicho ya kuboresha maisha yao.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho wilayani Mbozi mkoani Songwe juzi, Wasira alisema kazi kuu ya chama hicho ya kuondoa maradhi , ujinga na umaskini na inaendelea kufanyika na kwamba utekelezaji wake ni wa muda mrefu.
“Tulipotangaza kwamba tuna maadui watatu , maradhi , ujinga na umaskini, tulikuwa tunatangaza vita ya kudumu ya mambo hayo na kujenga maisha yenye nafuu kwa watanzania” alisema Wasira.
“Ili mradi watanzania wanatuamini Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwapo na hakuna dalili za Watanzania kutokuendelea kutuamini mimi sijaziona” alisema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED