Chama cha ACT Wazalendo kimezindua rasmi mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa chama hicho katika kanda nne za Tanzania, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Katika uzinduzi huo, viongozi wakuu wa chama walihusika moja kwa moja na shughuli hiyo kwa kufungua rasmi mafunzo katika maeneo mbalimbali.
Kanda ya Kusini ilizinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama upande wa Bara, Isihaka Mchinjita, katika wilaya ya Masasi. Kwa upande wa Kanda ya Kati, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaib, aliongoza uzinduzi wa mafunzo hayo.
Katika Kanda ya Ziwa, Naibu Katibu Mkuu wa chama, Ester Thomas, alifungua rasmi mafunzo hayo, huku Kanda ya Kaskazini ikizinduliwa na Kiongozi wa chama mstaafu, Zitto Kabwe.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaandaa viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali kuelekea uchaguzi, sambamba na kuwajengea uwezo wa kulinda misingi ya demokrasia. Viongozi hao walipewa maelekezo ya namna ya kujiandaa kwa mapambano ya kisiasa, kwa kutambua kuwa mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana bila jitihada na ujasiri, hasa mbele ya chama tawala – CCM – ambacho kinaelezwa kuwa hakitakubali kuondoka madarakani kwa urahisi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED