SHILINGI bilioni 2.9 zinatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta yatokanayo na mbegu za zao la pamba, kinachotarajia kuanza ujenzi wake mwezi februari mwaka huu huku kikitarajia kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja.
Aidha, kiwanda hicho kinajengwa na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama(KACU) katika mtaa na kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) hivyo kila mkulima atakayekiuzoa pamba chama hicho atalipwa malipo ya pili.
Mwenyekiti wa Chaka hicho Emmanuel Nyambi aliyabainisha haya jana wakati wa kukabidhiwa magari mawili yenye thamani ya Sh.milioni 380 ambazo zinatokana na mkopo wa ujenzi wa kiwanda zitazotumika kubeba pamba,halfa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha.
Alisema, msimu wa kilimo wa 2024/2025 wamepokea mkopo wa Sh.bilioni 2.9 kutoka Benki ya Maendeleo ya kilimo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta yanayotokama mbengu za zao la pamba ili kuongeza uzalishaji wake, ajira kwa vijana wanaowazunguka, uchumi wa wakulima kwa kulipa malipo ya pili na mapato ya serikali yanayotokana na pamba.
Nyambi alisema kati ya fedha hizo Sh.Bilioni 1.159 zitatumika katika ujenzi wa kiwanda na usindikaji wa mitambo, Sh.bilioni 1.2 ununuzi wa mitambo, Sh.milioni 142 gharama za ulipaji bandarini pamoja na Sh.milioni 380 zilizotumika katika kununua magari mawili ya kubeba zao hilo yenye na kuahidi kiwanda kukamilika kwa wakati na kuanza kazi yake.
Mbunge wa jimbo Ushetu na Mwenyekiti matafu wa chama hicho Emmanuel Cherehani alisema,ili kuongeza uzalishaji wake pia waongezee maaofisa ugani watakaowafikia wakulima na kuwakumbusha kununi 10 za kilimo na kupata pamba safi na bora itakayoshindana kwenye masoko ya kimataifa.
Alisema,kwakuwa anakiwanda cha kuchakata zao hili mbengu zinazopatikana atakuwa anakiuzia kiwanda hicho ili kisikose malighafi na kuhakikisha wakulima wanapata malipo ya pili yatakayowahamasisha kulima kwa tija na kupata fedha za kuinua uchumi wao.
Awali Ofisa Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) Andrew Ezekiel alisema,wameanza kukikopesha chama hicho fedha tangu msimu wa kilimo wa 2020/2021 kwa mkopo wa Sh.Bilioni 4.6 na walizitumia vema katika lengo lililokusudiwa na kuurejesha kwa asilimia 100.
Alisema,msimu huu wa 2024/2025 wamewapatia mkopo wa Sh.bilioni 2.9 za ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta yanayotokana na mbengu za pamba na kuwataka kutumika kwenye matumizi yaliyopangwa ili kitakapokamilika kilipe malipo ya pili kwa wakulima wake, ajira kwa vijana wanaowazunguoa na kulipa zaidi mapato ya serikali yanayotokana na zao hilo.
Ezekiel alisema, awali kacu ilikuwa inauza pamba mbegu zilizoshuka uzito kwa gharama ndogo kulinganisha na gharama za uchumbuzi wake sasa watakuwa wanakamua wenyewe na kuuza mafuta yake na kiwanda hicho kinachokwenda kujengwa kitakuwa cha mfano nchini na kusisitiza kutunza mitambo yake ili kiendelee kuwanufaisha wakulima wote.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha alisema,katika moja ya kazi aliyopewa na Rais Dk.Samia Suruhu Hassani ni kuinua zao la pamba hivyo kiwanda hicho kitasaidia kuongeza uzalishaji wake na kulipa malipo ya pili kupitia pamba zinazopatikana baada ya kuzichambua na kuuza pamba nyuzi pamoja na mafuta yake yatakayopatikana.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED