Rais Mwinyi amuapisha Kamishna ZRA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:11 PM Feb 12 2025
Kamishna Mkuu Mpya wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Said Kiondo Athumani.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kamishna Mkuu Mpya wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Said Kiondo Athumani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Kamishna Mkuu Mpya wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Said Kiondo Athumani aliyemteuwa hivi Karibuni.

Hafla hiyo imefanyika Ikulu  Zanzibar na Kuhudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla,Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Kabla ya Uteuzi huo Kamishna Kiondo alikuwa Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Kodi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA).