WALENGWA wa TASAF katika Manispaa ya Ilemela waeleza walivyoimarika kiuchumi mara baada ya kufanikiwa kuanzisha miradi ya ujasiliamali inayowaingizia kipato na kuiendesha kwa ufanisi.
Laurensia Lubigisa ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Usikivu anaeleza kuwa kikundi chao walipata ufadhili wa TASAF kupitia mradi wa kupunguza umaskini (OPEC) kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji wa biashara, hivyo wanajihusisha na utengenezaji sabuni za maji, miche na unga wa lishe.
Naye Mkurugenzi wa Mifumo, Tathmini na Mawasiliano kutoka TASAF Makao Makuu Dodoma Japhet Boaz, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF mara baada ya kukagua miradi inayotekelezwa na wanachama hao.
Alisema wanatekeleza miradi ya ujasiliamali kwa walengwa hao ambao wametoka kwenye hali duni ili waweze kujijenga na kupata ruzuku kupitia mpango huo na utakaowawezesha kupata vipato vya uhakika.
"Wameweza kuendesha vikundi na kukopeshana wao kwa wao na vimeweza kusaidia wengi hasa kwenye kuongeza vipato na wanaweza kujadili mambo mbalimbali ambayo yatasaidia katika mfumo mzima wa maisha" alisema.
Aliongeza kuwa wanaishukuru serikali kwa sababu kwa kuwainua wananchi kutoka kwenye hali duni na kuipanda kwenye maisha yenye unafuu wa kupata huduma hizo za kijamii.
Naye Mtaalamu wa Hifadhi ya Jamii kutoka Benki ya Dunia Tumainiel Ngowi anaeleza kuwa wameridhika kwa kiasi kikubwa mara baada ya kuona jitihada zilizofanywa katika kuboresha maisha wanufaika wa TASAF na hiyo inawapa moyo na motisha wa kuendelea kupigana vita na umaskini katika kaya husika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED