Wizara ya Fedha imeanza kutoa mafunzo kwa wananchi ili kuwasaidia kuepuka mikopo umiza na migogoro ya kifedha katika jamii. Mafunzo hayo yanafanyika katika Kata ya Makanya, Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Ofisa Usimamizi wa Fedha wa Wizara hiyo, Stanley Kibakaya, amesema migogoro mingi ya kifedha inatokana na watoa huduma wasio waaminifu, ukosefu wa taarifa sahihi kwa wateja, na uelewa mdogo wa wahudumu wa huduma za kifedha kuhusu wajibu wao.
Hatua hii inalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika masuala ya kifedha ili kupunguza migogoro na changamoto zinazotokana na mikopo kandamizi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED