Yas Tanzania yaibuka kidedea tuzo za TEHAMA 2025

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 10:20 PM Feb 22 2025
Yas Tanzania yaibuka kidedea tuzo za TEHAMA 2025
Picha: Mpigapicha Wetu
Yas Tanzania yaibuka kidedea tuzo za TEHAMA 2025

KATIKA kutambua mchango mkubwa wa uwekezaji , utoaji huduma na ubunifu, kampuni ya huduma za simu ya Yas Tanzania leo imetunukiwa tuzo tatu katika sekta ya Tehama.

Katika tuzo hizo za Tehama zilizotolewa jijini Arusha, Yas imeshinda katika kipengele cha Huduma bora za Intaneti (Best Internet Service Provider).

Tuzo nyingine waliyoishinda ni tuzo ya Kampuni Bora ya  Mawasiliano Tanzania (Best Mobile Network Provider) na tuzo ya Mtumiaji Bora wa Tehama na Manufaa kwa Jamii.

1

Tuzo zimetolewa kwenye ukumbi wa Gran Melia jijini Arusha.