JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limemkamata na kumfungia leseni ya udereva kwa miezi mitatu dereva wa gari ya serikali lenye namba za usajili STN 6256 aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.
JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limemkamata na kumfungia leseni ya udereva kwa miezi mitatu dereva wa gari ya serikali lenye namba za usajili STN 6256 aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni, imeeleza kuwa dereva Kassimu Ludohela (32) alikaidi amri ya kusimamishwa Morogoro kwa kosa la kuyapita magari mengine sehemu. isiyoruhusiwa kisheria
"Dereva huyo ambaye Aprili 01, 2025 katika eneo la Kihonda Darajani, Mkoani Morogoro alisimamishwa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani na kuelezwa kosa lake alilolitenda, wakati askari akichukua taarifa za gari dereva huyo alirudisha gari nyuma na kuendesha kwa kasi kwenda mbele," amesema.
Tukio hilo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
"Polisi Mkoa wa Dodoma, inatoa rai kwa madereva wote kuheshimu na kufuata sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka ajali hatua nyingine zitachukuliwa dhidi yake," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED