Tanzania na Angola zimetia saini hati za makubaliano zinazolenga kudumisha sekta uchumi, na mambo ya kiusalama yenye kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo yatakayofungua fursa za biashara za uwekezaji na kuimarisha ulinzi na usalama yametiwa saini na mawaziri wa Ulinzi Tanzania, Dk. Stagomena Tax na Waziri wa Ulinzi wa Angola, Jenerali (mstaafu) Joao Ernest Dos Santos kwa niaba ya marais wao.
Makubaliano yameingiwa wakati Rais Samia akiwa katika ziara ya siku tatu Luanda, nchini Angola yanayo dumisha ushirikiano wa kihistoria uliowekwa na waasisi wa nchi hizo mbili, Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Angola, Hayati Antonio Agustino Neto.
Wakizingumza na waandishi wa habari leo baada ya mazungumzo ya faragha, Ikulu ya Luanda, Rais Samia Suluhu Hassan, amesema wamekubaliana mambo kadhaa yakiwamo ya hali ya kisiasa na uchumi wa nchi zao.
Amesema Tanzania ina nia ya kuimarisha ushirikiano wao ili kuondoa hofu katika maendeleo ya kiuchumi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED