Martha Karua azuiwa 'Airport'

By Enock Charles , Nipashe
Published at 09:56 AM May 18 2025
Mwanasiasa kutoka nchini Kenya ambaye pia ni Wakili, Martha Karua
PICHA: MTANDAO
Mwanasiasa kutoka nchini Kenya ambaye pia ni Wakili, Martha Karua

Mwanasiasa kutoka nchini Kenya ambaye pia ni Wakili, Martha Karua amedai kuzuiwa kuingia nchini baada ya kufika katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akiandika katika ukurasa wake wa X, Karua ameeleza kwamba yeye na wenzake wamefika katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere lakini wakazuiwa kuendelea na safari yao wakitakiwa kurudi walipotoka kwa sababu ambazo bado hazijawekwa bayana.

Kwa mujibu wa taarifa ya John Mnyika, Martha Karua alikuwa ahudhurie kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu katika mahakama ya Kisutu kesho pamoja na wanasheria wengine kutoka Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kusikiliza kesi inayomkabili.

Lissu alifunguliwa mashtaka ya Uhaini na kesi yake inatarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku kwa mara ya kwanza wafuasi wa chama hicho wakiruhusiwa kwenda mahakamani kusikiliza shauri la Mwenyekiti wao.