Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kujifunza mambo yanayohusisha masuala ya kiteknolojia ili waweze kuendana na kasi ya utandawazi.
Ushauri huo umetolewa Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampuni ya SpiddTZ ambayo imekuja nchini kwa lengo la kurahisisha teknolijia.
Meneja Maendeleo wa Kampuni hiyo, Catherine Kusaka, amesema lengo la kuja hapa nchini ni kuleta teknolijia katika eneo la ufanyaji kazi kidijiti pamoja na kusaidia kukuza kampuni kwa kutumia teknolojia.
"Tumetokea Uganda tumekuja Tanzania kuwekeza kwakuwa tumeona bado matumizi ya teknolojia ni madogo ukilinganisha Kenya na Uganda ndio maana tumeamua kuleta kampuni hii ili kusaidia katika eneo hilo" amesema
Ameongeza ujio wa kampuni hiyo utawezesha watanzania kupata urahisi wa kiteknolojia na vijana wengi kupata ajira.
"Huduma hii kwa Sasa imeanza kutolewa Dar es Salaam tukiona mapokeo mazuri ndio tutaifikia mikoa mingine tumeona bado kuna kampuni zinatumia karatasi, wengine kufanya mkutano lazima wakutane lakini sisi katika huduma zetu tunaleta urahisi wa kuwakutanisha kwa kutumia teknolojia hata kama mtu yupo katika mkoa tofauti" amesema
Menajea Mkuu wa Kampuni hiyo, Angera Somwegerere amesema huduma zinazopatikana nchini kwa sasa zinajumuisha kusaidia biashara, kujenga mitandao ya kuaminika inayoweza kusambazwa na yenye utendaji wa juu ambayo inakidhi mahitaji ya mabadiliko ya kidijitali katika sekta zote.
Aliongeza pia teknolojia tuliyonayo itasaidia kurahisisha shughuli mbalimbali katika Benki, hospital, viwandani na kwenye taasisi nyingine kubwa zinazotumia huduma za kidijitali.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED