Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amosi Makalla amesema ilani ya chama hicho imetekelezwa kwa kiasi kikubwa na ukweli wake unadhihirika kutokana na maendeleo yaliyogusa kila sekta.
Amesema hilo linawapa nguvu na imani kwa wananchi kwamba chama hicho kiliahidi na kimetekeleza kwa vitendo na kwamba hata ilani nyingine itakayokuja itagusa zaidi maisha ya watu na kukifanya chama hicho kushinda.
Makalla ameyasema hayo leo Mei 17 alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu utakaofanyika Dodoma mwishoni mwa mwezi huu (29-30) ambao umelenga mambo matatu yakiwamo:
Kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya miaka mitano kuanzia Mwaka 2020-25, kuzindua ilani mpya ya Uchaguzi kuanzia Mwaka 2025-30 na kufanya marekebisho madogo katika Katiba ya chama hicho.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED