SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limemsamehe na kumrejeshea zaidi ya ng’ombe 500 Mzee Igembe Mahola mkazi wa Kijiji cha Iyala Kata ya Luhanga katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambaye alikuwa anachungia mifugo hiyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Mzee huyo amekabidhiwa mifugo hiyo na maofisa wa TANAPA baada ya taratibu za kisheria kukamilika ambapo ameahidi kutorudia tena kuchungia mifugo kwenye hifadhi hiyo.
Ofisa Uhusiano wa TANAPA, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Catherine Mbena amesema vitendo vya wafugaji kuingiza mifugo hifadhini kinasababisha uharibifu wa ikolojia ya hifadhi hiyo na kukwamisha shughuli za uhifadhi.
Amewataka wafugaji kuacha kuingiza mifugo hifadhini na kwamba msamaha uliotolewa kwa mzee Mahola hautatolewa tena kwa watakaokamatwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED