Mashabiki wa timu ya Simba wakiongozwa na mwanadada aliyejizoelea umaarufu mitandaoni kwa kuishabikia timu hiyo, Agnes Daniel maarufu Aggy Simba wamefanya dua ya kuiombea timu ishinde mechi ya leo ya hatua ya kwanza ya fainali dhidi ya berkane pamoja na kutoa sadaka kwa watu wenye uhitaji.
Akizungumzia wakati wa kukabidhi mahitaji hayo katika kituo cha Furaha na Amani mkoani Dar es Salaam amesisitiza kwamba Mungu hupokea dua za watu wanaopenda kusaidia watu wenye uhitaji.
"Wakati uliopita tulikuwa katika kituo cha watoto yatima Zanzibar tulitoa msaada lakini safari hii tumekuja hapa na hii yote ni kumshukuru Mungu kwa hatua ambayo timu ya Simba imefika.
"Tuko fainali leo tuna mechi ya fainali kabla ya kufika hatua hii tulimuomba Mungu tufike nusu fainali na sasa tunamuomba Mungu katika hii fainali tushinde ili Simba iwe timu ya kwanza kuleta kombe la Afrika.
"Kama mashabiki ni jambo la kumshukuru Mungu sadaka ni jambo la kheri na sisi tumekuja kufanya jambo la kheri tunamuomba Mungu na kumshukuru ili tuweze kwenda katika hatua ambayo tunaitamani kama mashabiki wa Simba" amesema Aggy
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED