Makalla aeleza alipo Wasira

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 12:51 PM May 17 2025
Steven Wasira
PICHA: MTANDAO
Steven Wasira

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amosi Makalla amesema Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Steven Wasira yupo na kwamba haonekani kwa sababu ya ratiba tu.

Siku chache zilizopita zilienea taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba Wasira anaumwa hali ambayo ilizua taharuki kwa wafuasi wa chama hicho na wadau wengine wa siasa.

"Wasira yupo, Kuna muda mambo ya kifamilia na nini mbona mm nafanya ziara napumzika na kuwa na ratiba nyingine viako vya ndani vya ofisini mzee hana jambo lolote ni ratiba kwamba bwana nafanya hapa napumzika kidogo naenda kuona watoto kwahiyo ni jambo la kawaida" amesema Makalla