Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Chionda Kawawa amesema Nachingwea imebarikiwa kuwa na ardhi iliyosheheni madini na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mhandisi Kawawa alisema kuwa kutokana na uwekezaji wa kwenye migodi ya madini na kilimo kutachochea kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya ya Nachingwea.
Mhandisi Kawawa alisema kuwa uchumi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea unategemea kilimo na madini hiyo kufunguliwa na migodi mingi kutasaidia kukuza uchumi na kuwafanya wananchi wengi kuwa mabilionea kutokana na kukua kwa uchumi wa madini na kilimo.
Wananchi wa wilaya ya Nachingwea wametakiwa kuchangamkia fursa za kilimo na madini ni ili kufikia malengo ya viongozi wa wilaya ya Nachingwea kuwawezesha kuwa mabilionea.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED