Mbunge Mtaturu: Tuondokane na kadi nyingi zinavimbisha suruali

By Augusta Njoji , Nipashe
Published at 06:25 PM May 16 2025
Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu
PICHA: MTANDAO
Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu

Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu amesema utekelezaji wa mradi wa Tanzania kidigitali utasaidia mifumo kusomana na kuondokana na watu kutembea na kadi nyingi zinazovimbisha suruali.

Mtaturu ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2025/26.

“Huu ni mwelekeo wa kwenda kwenye e-card tuachane na mtu kuwa na makadi mengi hadi yanavimbisha suruali kumbe huna fedha una makadi mengi mara ya NHIF, leseni, kitambulisho cha kura, huna fedha unakuwa umejaza makadi mengi, ikienda ikapatikana e-card tutaondokana adha hii,”amesema.