Huwezi kuzuia uchaguzi ukiwa nje ya uchaguzi

By Enock Charles , Nipashe
Published at 11:41 AM Apr 06 2025
John Mrema
Picha: Imani Nathaniel
John Mrema

KUNDI cha watia nia 55 (maarufu kama G55) limesema dhana ya no reforms no election ilianza 2020 na CHADEMA ikashiriki Uchaguzi wa Mkuu 2020 na Uchaguzi wa Serikali Mitaa 2019.

Limesema, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hichoi taifa, Freeman Mbowe, alisema maamuzi sahihi yatafanyika, sio kuzuia uchanguzi.

"Kama tungetaka zuia uchnaguzi tungezuia na uandikishaji wapigakura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, ambao umeshafanyika nchi nzima. 

"Madhumini ya chama ni kushika dola.. chama sio pressure group.. haki za wananchama wanaotaka kugombea wananyima haki wanachama wanaotaka kuombea. 

Akizungumza kwa niaba yao, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amesema vyama vingine vinashiriki uchaguzi na kwamba viongozi hawajafanya jitihada ya kuunganisha nguvu na kwamba madhara ya kutoshiriki ni makubwa kuliko faida. 

"Viongozi wa dini na madhehebu wanaendelea na kuhamisha waumini kushiriki ama chama kimechelewa au kimekwama kupata uungwaji mkono, viongozi wa dini wanakubali ‘reforms’ lakini hakuna anayehimiza waumini wasishiriki, maana yake hawajakubaliana na sisi au hajashawishiki," amesema Mrema.

Aidha, Mrema amesema lengo si kufanya uasi na kuvunja katiba, na kwamba wadau wao wanaunga mkono ‘reforms’, lakini hawaungi mkono kuzuia uchaguzi.

“Ni kama wamepoa hawaamini kwenye kuzuia uchanguzi. Chama kitapoteza kabisa ruzuku, tulikuwa na hali ngumu kuendesha chama. 

“Wakawa wanabeza chama sio ruzuku, sawa, Je kampeni ya ‘Tone Tone’ imefika wapi? Viongozi hawasemi, kwa sababu hawana cha kusema. Athari tumeiona na tumekishauri chama," amesema.

Mrema amesema: "Upo uwezakano wa kushirki na kushinda uchaguzi pamoja na hujuma, yapo madhaifu ndani ya chama madiliko ni 'process' wagombea sahihi, tutawashinda uchaguzi.

 

"Kuzia uchaguzi kutamwaga damu. Wapo wanaojenga hoja kwamba kushiriki ni kupeleka vijana wakamwage damu. Udikekta unaanza kushamiri CHADEMA

“Kuna harakati za kunyamazisha sauti kinzani, tulipinga udiketa nje ya ndani ya nchi, ilhali sisi ndani ya chama tunafanya.”