MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amewasisitiza walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo, kufanya kazi kwa bidii na weledi katika kufundisha wanafunzi shuleni, ili kuinua ufaulu wao na kushika nafasi nzuri kitaifa.
Amesema kwamba muda mrefu mkoa huo hauna matokeo mazuri.
Amebainisha hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Wadau wa Elimu mkoani humo na kufanya tathimini, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga Butengwa.
Amesema mkoa huo wa muda umekuwa haufanyi vizuri kitaifa katika kufaulisha wanafunzi na kuwataka walimu waongeze bidii katika ufundishaji wao, ili kuongeza ufaulu na hata kushika nafasi nzuri kitaifa.
Baadhi ya walimu hao, wamemuahidi Mkuu wa Mkoa kwamba, watakwenda kuyafanyia kazi maagizo yake, iili kuhakikisha kwamba mkoa huo, unapiga hatua katika elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED