Sharifa atangazwa Mwenyekiti BAWACHA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:34 AM Jan 18 2025
Sharifa Suleiman.
Picha: Mtandao
Sharifa Suleiman.

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Zanzibar na baadae kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman, ameibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza hilo baada ya matokeo kutangazwa.

Sharifa ameshinda kwa kura 222 sawa na asilimia 62% dhidi ya mpinzani wake Celestine Simba ambaye amepata kura 139 sawa na asilimia 38% ya idadi ya wapiga kura ni 382 huku halali zikiwa 361 na zilizoharibika zikiwa 2.

Sharifa ameshinda baada ya uchaguzi kurudiwa kutokana na matokeo ya awali kutokuwa na mgombea aliyefikisha kura zaidi ya asilimia 50%.

Elizabeth Mwakimomo ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Bara.

Mwanzo nafasi hiyo iligombaniwa na watu saba lakini hakuna aliyefikisha kura asilimia 50% baada ya uchaguzi kurudiwa Elizabeth Mwakimomo alipata kura 212 sawa na asilimia 59% huku mpinzani wake Salma Kasanzu akipata kura 147 sawa asilimia 41%.