Tanzania, Hungary kushirikiana katika kuboresha sekta ya maji nchini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:26 PM Oct 05 2024
Tanzania, Hungary kushirikiana katika kuboresha sekta ya maji nchini
Picha: Mpigapicha
Tanzania, Hungary kushirikiana katika kuboresha sekta ya maji nchini

Waziri wa Maji, Juma Aweso na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mha. Mwajuma Waziri wamekutana na Balozi wa Hungary mwenye makazi yake Nairob Kenya Zsolt Meszaros akiwa na ujumbe kutoka Hungary.

Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za DAWASA Dar es Salaam kimelenga kupanua wigo wa Mashirikiano na Serikali ya Hungary hususani katika sekta ya Maji. 

Aidha, Balozi huyo ameeleza ya Kwamba nchi yake inatoa mikopo  isiyokuwa na riba kupitia programu ya Hungarian Tied End Credit, l Balozi Zsolt akifafanua zaidi amesema kupitia programu hiyo Tanzania itanufaka eneo la uwekezaji kwenye sekta ya Maji.

1

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemueleza Balozi ya kuwa Wizara ya Maji ipo tayari Kwa ajili ya Mashirikiano katika kuhakikisha lengo la kumtua Mama ndio kichwani linatimia kwani ndio kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.