"Uwekezaji Cocobeach iwe mfano kwa wawekezaji wa ndani" Prof. Kitila

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 04:54 PM Oct 05 2024

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo
Picha: Mauld Mmbaga
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema uwekezaji uliofanywa katika eneo la Bravo Cocobeach ikawe mfano kwa wawekezaji wa ndani, huku akizitaka mamlaka za serikali za mitaa kuwa sehemu ya kuvutia wawekezaji, kuondoa vikwazo na kuwezesha shughuli za kiuchumi.

Waziri Mkumbo ametoa rai hiyo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa uwekezaji wa Bravo uliopo eneo la Cocobeach Kinondoni Jijini Dar es salaam lililobuniwa na kuhifadhiwa na muwekezaji wa ndani.

Pamoja na kukoshwa na ubunifu wa mandhari na utoaji huduma Prof Mkumbo amesema;  "Eneo hili litumike kama mfano kwa wawekezaji wa ndani na halmashauri zingine ziige mfano wa Kinondoni na Watanzania wengi even waendelee kujitokeza kuwekeza kwenye maeneo yenye tija".