UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Shinyanga Mjini, umeendelea na ziara ya Kata kwa Kata ya kuhamasisha vijana, wanachama wa chama hicho na wananchi, kuwa wajiandae kwenye Uchaguzi Mkuu 2025.
Pia umesema, vijana hao wampigie kura nyingi Rais Samia Suluhu Hassan na wagombea wote wa CCM.
Ziara hiyo imeanza jana, ambayo ina kauli mbiu isemayo ‘Mama Full Box Oparesheni’ ikiwa na maana kura za Rais Samia, zijae kwenye sanduku la kura siku hiyo ya uchaguzi, ili apate ushindi wa kishindo na kuendelea kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo.
Pia, pamoja na Dk. Emmanuel Nchimbi, kuwa mgombea mwenza.
Amesema kutokana na kuunga mkono Azimio hilo, wameamua kufanya ziara ya kuhamasisha vijana, wana-CCM na wananchi wajiandae na uchaguzi mkuu.
Aidha, amesema Kata ya Mwawaza kunakamilishwa ujenzi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga, ambayo sasa inajengwa barabara ya kiwango cha Lami.
Pia, amewasihi wanachama wa chama hicho kwamba kipenga cha kuchukua fomu kitakapotangazwa nafasi ya udiwani na ubunge, wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu na kugombea nafasi hizo, kwa kujipima kwanza kama wanatosha kwenye nafasi hizo.
Katika ziara hiyo ya ‘Mama Full Box Oparesheni’ ina ambatana pia na uzinduzi wa Mashina ya Mama".
Picha: Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdulazizi Sakala, akizungumza kwenye ziara hiyo ya ‘Mama Full Box Oparesheni’ Kata ya Mwawaza.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED