Mashirika ya ndege yashitukia chanzo moto, marufuku kubeba ‘power bank’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:26 PM Mar 26 2025
Mashirika ya ndege yashitukia chanzo  moto, marufuku kubeba ‘power bank’
Picha: Mtandao
Mashirika ya ndege yashitukia chanzo moto, marufuku kubeba ‘power bank’

KUNA lawama sasa kwamba kuna hatari ya vyanzo moto katika usafiri wa ndege, wanapokwa wamebeba ‘power bank,’ ikitajwa sasa kuwa chanzo cha moto kwenye ndege aina ya Airbus A321 nchini Korea Kusini.

Mamlaka za eneo hilo hazijasema moto huo ulisababishwa na 'power bank'. Vilevile, ndege aina ya Air Busan ikashika moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gimhae nchini Korea Kusini Januari 28, mwaka huu. Watu watatu walijeruhiwa kidogo.

Wizara ya Uchukuzi ya Korea Kusini, inasema mnamo Machi 14 mwaka huu, uchunguzi ulibaini kuwa ‘power bank’ iliharibika na kusababisha ndege hiyo kushika moto.

Inatajwa kuwa, ‘power bank’ hiyo ilikuwa kwenye eneo la kuhifadhi mizigo juu ya kiti cha abiria, ambako ulizuka moto kwa mara ya kwanza.

Wadadisi wanasema kwamba kifaa hicho kilionyesha dalili za moto, lakini haijulikani kwanini betri ya ‘power bank’ iliharibika.

Jambo kuu ni kwamba, Ripoti ya Uchunguzi wa muda mfupi tu. Ripoti ya mwisho ya uchunguzi, kuhusu ndege hiyo bado haijatolewa.

MARUFUKU 2016 

Mashirika ya ndege duniani kote sasa yamepiga marufuku ‘power bank’ kubebwa kwenye mizigo inayoingia (vitu unavyokabidhi kabla ya kupanda ndege) kwa miaka mingi kwa sababu za kiusalama.

‘Power bank’ zina betri aina ya ‘lithiamu-ioni’ na betri hizo zina uwezo wa kuzalisha joto kubwa, hata kusababisha mshituko wa umeme. Hapo  inatajwa kiufundi kwamba, kukiwapo kasoro yoyote ndani yake, inajenga hatari ya moto.

Kwa ushauri uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA), tangu mwaka 2016, abiria wamepigwa marufuku kubeba betri zozote za ‘lithiamu-ion’ kwenye mizigo iliyokaguliwa kwenye ndege.

Hiyo ni kutokana na moto uliozuka kwenye ndege Airbus nchini Korea Kusini, kampuni hiyo Air Busan imeanza kuchukua hatua za kiusalama, ikitangaza abiria hawataruhusiwa tena kubeba power bank kwenye mizigo yao ya mkononi.

Kampuni hiyo inasema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuongezeka matukio ya ‘power bank’ kupata joto.

Wakati huohuo, mashirika ya ndege, China Airlines na Thai Airlines pia zinatekeleza sheria kama hiyo.

Scoot, shirika la ndege la gharama nafuu la Singapore Airlines, nalo linatarajia kupiga marufuku matumizi na kuzichaji ‘power bank’ kwenye safari za ndege kuanzia Apili Mosi mwaka huu.

Mnamo Februari 28 mwaka huu, serikali ya Korea Kusini ilitangaza kwamba abiria wanaopanda ndege za ndani wanapaswa kukaa na betri zao na chaji, badala ya kuzihifadhi kwenye masanduku ya juu ndani ya ndege.

Yote inachangiwa na kuwapo matukio ya moto, hata kwenye meli yanayosababishwa na betri za lithiamu hapo awali.

Mnamo Machi 2017, headphones za mwanamke zililipuka kwenye ndege kutoka Melbourne, Australia, hadi Beijing. Ilisababisha jeraha usoni mwake. 

Inaelezwa mkasda ulivyokuwa, mwanamke huyo alizinduka baada ya kusikia ‘headphone’ zake zikilipuka na mara moja akazivua na kuzitupa chini.

Baada ya ajali hiyo, ilibainika kuwa ajali hiyo ilisababishwa na hitilafu katika betri ya ‘lithium-ion’.

Hapo awali, safari ya ndege huko Sydney Australia, ilisitishwa baada ya moshi kuonekana kutoka eneo la mizigo.

Baadaye iligundulika kuwa betri ya ‘lithiamu-ioni’ iliyohifadhiwa kwenye mizigo na ilikuwa imepata moto.

Jumuiya ya Huduma za Mazingira ya Uingereza ilisema katika ripoti yake yam mwaka 2022, ukatamka kwamba kuna matukio 700 ya moto yanaripotiwa kila mwaka katika sehemu za kutupa taka, mengi chanzo chake ni betri za ‘lithiamu’ zilizotupwa.

Betri za hizo za ‘lithiamu-ion’ zinaweza kulipuka ikiwa zimeharibiwa au kuvunjika. Betri hizo hazitumiwi tu katika ‘power bank’, bali pia katika miswaki ya betri, vinyago, simu za mkononi na kompyuta mpakato.

JIJUE BETRI ‘LITHIAMU’

Betri za ‘lithiamu’ aina ya ‘BSLBATT’ zinatajwa hutoa nishati zaidi kwa matumizi ya juu kuliko betri zilizozoeleka, za nguvu itokanayo na tindikali ya risasi.

Pia, hutoa chaji na zina ufanisi mkubwa, inadumu na kutokuwa na matengenezo ya kila mara!

Hata kiutendaji, betri hizo zinatajwa kushika soko zikiwa na ‘lithiamu’ nyingi kila moja ikichukua nafasi ya betri ya risasi maradufu.

Inatajwa kuwa na nguvu inayoweza kutumika hata mara nane hadi 10 zaidi katika kasi yake ya kuchaji iko juu sana.

Pia, betri zake hutumika vyema zaidi zinapochajiwa hata na nyenzo za jua na hata inapokuwa nje ya chaji, inakuwa na uwezo katika hali kama inayo chaji, kuweza kutumika