Baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wamewapongeza waandaaji wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon kwa kitendo cha kuongeza muda wa zoezi la uchukuajinamba na tisheti za kukimbilia kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu yatakayofanyika Jumapili Mjini Moshi.
Wamezungumza wakati zoezi hilo limeingia katika siku ya pili katika Hoteli ya Kibo Palace na linatarajiwa kumalizima Jumatano jioni.
“Hili ni jambo jema sana kwani hapo nyuma muda ulikuwa mfupi mno tunashukuru wamesikiliza maoni yetu na kuongez amuda,” alisema Bw, Jacob Mollel aliyenda kwa ajili ya kumuandikish mjukuu wake katika mbio za KM 5 (Fun Run).
Naye Jackline Werema alisema, “Mbio nyingine zinatakiwa kujifunza kwa Kilimanjaro International Marathon kwani wanafanya mambo yao kwa mpangilio na weledi mkubwa unaona mwaka huu wameongeza muda ni jambio zuri sana.”
Kwa mujibu wa waandaaji, kituo cha mwisho cha zoezi hilo kitakuwa Moshi Alhamisi (Februari 20) kuanzia saa 6 mchana hadi saa 11 jioni, Ijumaa (Februari 21) kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na Jumamosi (Februari 22) kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
"Tumeongeza muda hadi jioni ili kuhakikisha kwamba washiriki wanaweza kuchukua namba zao baada ya kazi na kupunguza foleni," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo, na kuongeza kwamba itakuwa rahisi zaidi kwa washiriki kuchukua namba zao katika kumbi za Dar es Salaam na Arusha ili kuepuka msongamano dakika za mwisho Moshi.
Kwa mujibu wa waandaaji, namba za Mbio za CRDB kilomita 5 bado ziko wazi na zinaendelea kuuzwa. Washiriki wanaweza kujiandikisha kupitia Mixx YAS (zamani Tigopesa) kwa kupiga *150*01#, kisha bonyeza 5 LKS, kisha bonyeza 6 (Tiketi) na fuata maelekezo ili kukamilisha usajili mtandaoni kupitia www.kilimanjaromarathon.com. Kumbuka, kuna idadi ndogo katika mbio hizi pia na tukio tayari limefanyika kwa zaidi ya asilimia 60, kwa hiyo usichelewe - wa kwanza kufika ndiye wa kwanza kuhudumiwa pia.
Waandaaji hao walitoa wito kwa washiriki kuzingatia muda uliotangazwa ili kuepusha usumbufu, na pia ametoa wito kwa wale wanaokusanya namba kwa marafiki au ndugu zao kuhakikisha wanapata nakala za vitambulisho vyao na barua za ridhaa zinazowaruhusu wawakilishi kuchukua kwa niaba yao.
Aidha, walitoa onyo kali dhidi ya wale wanaouza namba mtandaoni kinyume cha sheria, akisema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. "Hii ni kinyume cha sheria na tutawachukulia hatua za kisheria," alisisitiza.
Katika hili walengwa ni wale wanaokusudia kukimbia kwa kutumia namba feki, kwani watatolewa kwenye mbio, matokeo yao kufutwa na kufungiwa kushiriki mbio za Kimataifa za Masafa Marefu za Kilimanjaro Premium Lager.
Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hili ni tukio lisilostahimili kabisa aina yoyote ya uuzaji wa kuvizia, njiani, wakati wa tukio na kwa njia nyingine yoyote ya uuzaji, matangazo na ushirika wa chapa, na waandaaji watachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni au washiriki wowote wanaoonekana kuwakosea heshima wafadhili wao wakuu katika Mbio za Kimataifa za Masafa Marefu za Kilimanjaro Premium Lager, Masafa ya Kati ya Yas Kili, Mbio za Burudani za CRDB na pia wadhamini wao rasmi wanaowaunga mkono.
Wadhamini wa mwaka huu ni pamoja na Kilimanjaro Premium Lager – kilomita 42 (Mdhamini Mkuu), YAS- kilomita 21 Mbio za Masafa ya Kati, na Benki ya CRDB – Mbio za Burudani za kilomita 5. Wadhamini wengingine ni Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies and TPC Sugar, pamoja na wabia rasmi - GardaWorld Security, CMC Automobiles, Salinero Hotels – Kilimanjaro na wagawaji/watoaji - Kibo Palace Hotel na Keys Hotel.
Kili Marathoni huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na Executive Solutions Limited.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED