Vijana wenzangu, tuwe wenye busara katika kusimamia kanuni za mapenzi

By Tuntule Swebe , Nipashe
Published at 10:35 AM Sep 13 2024
Vijana wenzangu, tuwe wenye busara katika kusimamia kanuni za mapenzi
Picha:Mtandao
Vijana wenzangu, tuwe wenye busara katika kusimamia kanuni za mapenzi

NI jambo la kawaida sana, maisha na uhusiano au ndoa na uhusiano kuwa mzuri, pale wawili wanaporidhiana. Vilevile, pale yanapoingia doa, ndio panapogeuka kuwa tatizo.

Kwani kuna baadhi ya watu, waliokuwa kwenye uhusiano, huangukia kwenye kusaliti wenzi wao, wakaibuka na ama wanaume au wanawake wengine.

Mtu anayetendewa hivyo pindi anapogundua mwenza wake, anamsaliti huwa anumia na hapo ndipo fikra mpya zinajitokeza na akawa anaonekana kuwa na mtazamo hasi. 

Huwa wanapokumbwa na tatizo hilo, inawalazimu kuwa wakali kupita kiasi   na hata wanashindwa kudhibiti hasira. Wanamaliza maumivu yao kwa watu tofauti na waliowakosea.

Katika hilo, kuna wengine wanaofikiria hatua ya kujiua. Wanaofanya hivyo wako katika matazamo walichotakiwa ni kulitatua tatizo hilo, kupitia namna hiyo. Lakini, jibu linabaki kwamba, hiyo haikuwa sahihi, kwani ina hasara.

Tumeona watu wengine wakiwa na upweke, huku baadhi yao wanakosa hasara ya kupoteza wapendwa wao, waliokumbwa na matatizo ya namna hiyo.

Sambamba nao, wapo wanaopata matatizo ya afya ya akili, kwa sababu tu ya hilo la mvurugano kimapenzi, wakifikia hatua ya kuongea peke yao na baadhi ya hatua isiyo sahihi kibinadamu.

Chanzo kinabaki kuwa mapenzi. Hivyo, tukibaki pasipo kulitafakari hilo, ni kwetu jamii tunapoteza mwelekeo na kwa tafsiri pana tunaunda taifa tegemezi.

 Nakumbuka hadithi, kulikuwapo watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen (23) wakazi wa mkoani Katavi, wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikiitwa wivu wa mapenzi. 

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, mwaka jana, ambapo marehemu wote wakakutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti husika akakaririwa, amesema marehemu hao walikutwa na madhila wakiwa wanarudi nyumbani, kutokea kijiji chao kiitwacho Kabungu, walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, , akasema wanawashikilia watu wawili kuhojiwa, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya ‘wivu wa kimapenzi’, kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

 Kamanda huyo akaahidi kuwa Polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

Pia, kuna taarifa nyingine ya mwanafunzi wa chuo kikuu, ambaye jina lake halikuwekwa wazi, akaadaiwa kutaka kufanya jaribio la kujiua akiwa chuoni hapo. Chanzo kinatajwa ni masuala ya mapenzi.

 Ni tukio la Aprili 25, 2024 wakati alipokuwa katika moja ya majengo ya chuoni kwao na taarifa za awali, zikaeleza kuwa alipokorofishana na mpenzi wake, alitaka kujirusha kutoka juu ya ghorofa ya nne.

Ikaatarifiwa baadaye alikuwa amelazwa hosptalini, baada ya kuonekana hakuwa sawa.  

Ujumla wa hali halisi hiyo, ni kwamba  kuna haja ya elimu ya kina isambazwe baina ya wahusika wakifanya mazoezi ya Pamoja, wanashirikiana  na marafiki zao ili kuweza kusaidia mfumo wa afya ya akili  iende inavyopaswa, hali yenye msaada kwa kiasi kikubwa katika maisha ya jamii. Bila shaka, walio kwenye uhusiano wa kimapzi watazingatia haya yanayowahusu.

Hata hivyo, kwa wale waliopoteza wapenzi walioondoka katika maisha  ya duniani, inawapasa wasikate tamaa, waanze upya ulikukabiliana na hili uaminifu ni bora zaidi.