NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa ( NARCO) kuwandikia notisi ya kuondoka kwenye mashamba ya kuzalishia mifugo wawekezaji walioshindwa kuyatumia mashamba hayo kwa ajili mifugo.
Alitoa agizo hilo jana (Machi 8, 2025) mara baada ya kukagua mashamba ya kuzalishia mifugo Ranchi ya Kalambo iliyopo Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na kubaini baadhi ya wawekezaji wa mashamba ya kuzalishia mifugo wamekuwa wakiyatumia kwa shughuli za kilimo jambo ambalo ni kinyume na mkataba wa upangishaji.
Alisema serikali imetoa mashamba ya kuzalishia mifugo ili kuwasaidia wafugaji kupata maeneo ya malisho yatakayoongeza tija kwa uzalishaji wa mifugo bora na kuondoa migogoro baina ya wafugaji na wakulima.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED