CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa wananchi wa mkoani Mbeya kwa ajali iliyotokea jana jioni na kusababisha vifo vya wafu 28 na majeruhi, huku ikilitaka Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti matukio hayo nchini.
Kadhalika, imewataka madereva kuendelea kuelewa sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, akizungumza leo Juni 8, 2025, na wananchi wa USA River, wilayani Meru, mkoani Arusha, akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kaskazini, amesema:
“Jana jioni kulitokea ajali mbaya mkoani Mbeya tumepoteza watu 28, kati yao, 12 ni wanawake na kati yao watoto ni wawili na wanaume 16, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao na majeruhi ambao bado wanaendelea kutibiwa tunawaombea wapate nafuu,” amesema. Makalla amesema kauli mbiu ya CCM inasema, Kazi na Utu na hilo alilolifanya ni utu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED