Makalla: Nikiangalia vyama vya upinzani ni kama havipo

By Romana Mallya , Nipashe Jumapili
Published at 06:20 PM Apr 13 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla
Picha: Romana Mallya
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaambia watanzania wapime wenyewe, wapinzani badala ya wapinzania hao kwenda kwao kuwasaidia na kuwaomba mchango, huku wakiwakejeri.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, ameyasema hayo, leo, Aprili 13, 2025, Lindi Mjini, katika mkutano wa hadhara, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Makalla amewaeleza kuwa kwa sababu huwakejeri wanapokwenda kwao wasitoe mchango wanapowaomba.
Aidha, amesema udhaifu wa vyama vya upinzani, ni ushindi mkubwa wa CCM kwa sababu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chenyewe hakitoshiriki Uchaguzi Mkuu, CUF ni kama hawapo, huku ACT Wazalendo wakiendelea kuisha.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla
“Wenzetu wamepima, wameangalia kazi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakapima na wameona ushindi hawana wameamua kupumzika.

“CHADEMA hawatakuwapo kwenye uchaguzi wamepumzika. Sisi tunaamini udhaifu wa CHADEMA na vyama vingine ni ushindi mkubwa wa CCM. Nikiangalia vyama vya upinzani ni kama havipo,” anasema.

Makalla amesema CHADEMA wamepima na kuona kazi zilizofanywa na Rais Samia wameamua kupumzika.