Berta amwaga wino Arsenal Mkurugenzi mpya wa Michezo

By Vitus Audax , Nipashe Jumapili
Published at 03:17 PM Mar 30 2025
Andrea Berta (53) ametangazwa rasmi kuwa amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Arsenal kama Mkurugenzi wa Michezo.
PICHA: MTANDAO
Andrea Berta (53) ametangazwa rasmi kuwa amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Arsenal kama Mkurugenzi wa Michezo.

Andrea Berta (53) ametangazwa rasmi kuwa amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Arsenal kama Mkurugenzi wa Michezo.

Berta ambaye ametangazwa mapema leo Jumamosi 30 na klabu hiyo ya Uingereza amefanya kazi katika majukumu ya kiufundi katika nchi mbalimbali ikiwemo Italia Carpenedolo, Parma na Genoa huku hivi karibuni akitokea katika klabu ya Atlético Madrid.

Berta anatajwa kutumia takriban miaka 12 akiwa na Atléti akishika majukumu makubwa katika kuunda vikosi vilivyoshinda mataji ya LaLiga mnamo 2013/14 na 2020/21, na Ligi ya Europa mnamo 2018.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa nan a klabu hiyo ya Arsenal Mkurugenzi huyo amewahi pia kuiongoza Atléti  kushinda Copa Del Rey, UEFA Super Cup na Supercopa de España wakati pamoja na kufika fainali ya UEFA ya Ligi ya Mabingwa.

Andrea Berta ameeleza furaha yake kujiunga na Arsenal ikiwa katika kipindi cha muhimu zaidi ya kimafanikio ikitarajia kucheza mchezo wake dhidi ya Real Madrild katika robo fainali ya UEFA pamoja na mbio za ubingwa wa ligi kuu Uingereza EPL ambako bado iko nafasi ya pili ikitanguliwa na Liverpool.

"Nimetazama kwa shauku kubwa jinsi Arsenal ilivyobadilika katika miaka ya hivi karibuni na nimefurahia kazi ngumu ambayo imefanywa ili kuanzisha tena klabu kama nguvu kubwa katika soka la Ulaya na wafuasi wengi duniani kote.

 "Klabu ina maadili mazuri na historia nzuri, na ninatazamia kucheza sehemu yangu katika kuunda mustakabali mzuri na timu kubwa. "Siwezi kusubiri kuanza jukumu langu jipya na ninatazamia kwa hamu kucheza mchezo wangu wa kwanza kwenye Uwanja wa Emirates pamoja na wafuasi wetu,” amesema Berta.

 Mwenyekiti Mwenza wa Klabu hiyo Josh Kroenke amesema: "Yeyote anayejua soka anajua Andrea ni mtu wa kuvutia. Ana ujuzi mkubwa wa mchezo, rekodi nzuri ya kufuatilia, mtandao imara na hamu kubwa ya kujenga timu za ushindi.

"Andrea atakuwa nyongeza nzuri kwa klabu yetu. Anaelewa maadili yetu na kile tunachosimamia na hatuna shaka atatusaidia kusonga mbele na kuchukua hatua zinazofuata katika harakati zetu za kushinda mataji makubwa.

 "Tulifanya mchakato kamili wa kuajiri na tulifurahishwa sana na kiwango cha wagombea wengine wote, lakini ilikuwa uzoefu wa Andrea na mafanikio ambayo amefikia ndio yalionekana.

"Tunatazamia kufanya kazi pamoja na kumkaribisha katika familia ya Arsenal,” amesema Kroenke