TRA yakusanya trilioni 7.53 Januari hadi Machi 2025

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 01:32 PM Apr 04 2025
Kamishina Mkuu wa TRA,Yusuph Mwenda.
Picha: Mtandao
Kamishina Mkuu wa TRA,Yusuph Mwenda.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh.Trilioni 7.53 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha (Januari hadi Machi) 2024/2025.

Kamishina Mkuu wa TRA,Yusuph Mwenda, amesema hayo jana (Aprili 3, 2025) katika taarifa yake kwa umma kuhusu ukusanyaji mapato kuanzia Julai hadi Machi katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Amesema makusanyo hayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 101.32 ya lengo la kukusanya Sh.Trilioni 7.43 sawa na ukuaji wa asilimia 13.47 ukilinganisha na Sh.Trilioni 6.63 zilizokusanywa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

"Makusanyo yaliyokusanywa katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa 2024/2025  yamefanya TRA kuweza kuweka rekodi ya kipekee katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kufikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi sita mfululizo katika mwaka wa fedha," amesema katika taarifa hiyo.