Bodi ya Nyama Tanzania imewataka wamiliki wa bucha za nyama ya nguruwe (kitimoto) jijini Mbeya kuhakikisha wanazingatia matumizi ya vifaa stahiki katika usafirishaji, uhifadhi, na ukataji wa nyama hiyo.
Aidha, bodi hiyo imewasisitiza wamiliki wa bucha kudumisha usafi wa mazingira na vifaa wanavyotumia ili kulinda afya za walaji na kuhakikisha nyama inasalia katika hali bora kwa matumizi ya binadamu.
Wito huu unalenga kuboresha viwango vya usafi katika biashara ya nyama jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usalama wa chakula na afya kwa wananchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED