Msifate mkumbo barabarani-Mufti

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:06 AM Sep 17 2024
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana.
Picha: Mtandao
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana.

Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Alhaji Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally Mbwana amewataka Waislamu kote Nchini kuendelea kuhubiri amani na kuachana na vitendo viovu vitakavyopelekea uvunjifu wa amani ya Nchi.

Mufti amesema hayo katika Sherehe za Maulid ya Kitaifa iliyofanyika katika Viwanja vya Kalangalala Mjini Geita ambapo maelfu ya Waisalmu wamehudhuria akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini.

Mufti amesema “Mtume alikuwa Mtu wa subra, alikuwa Mtu wa pole, alikuwa akifundisha amani, Mungu alimtayarisha akawa ni Mtu wa namna hiyo hakufanya mambo ya kipuuzi hata siku moja”

“Na Mungu ametueleza katika Quran juu ya masuala ya amani ni ajabu Umma huu leo ikawa hawa ndio wanaovunja amani wao ndio wanaoharibu ulimwengu, msilete uharibifu, msieneze uharibifu katika Nchi,  Mungu ametukataza na Muislamu hatakiwi kila jambo ambalo linafanywa na anafanya na yeye”

“Tusisumbuliwe na Watu,  kikundi au fikra za baadhi ya Watu kwa makusudio yao.