DC Ndemanga: Tulindeni amani, tuepuke kujihusisha na maandamano

By Julieth Mkireri , Nipashe Jumapili
Published at 12:05 AM Dec 08 2025
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga
Picha:Julieth Mkireri
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga amewataka wananchi kushikamana na kudumisha amani iliyopo sambamba na kuepuka kuingia kwenye maandamano yatakayovuruga amani.

Ndemanga aliyasema hayo Desemba 6 alipokuwa akizungumza na Madiwani, watumishi na baadhi ya wananchi wa Halmashauri hiyo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani.

Aliwataka wananchi kuepuka kuunga mkono yanaoongelewa kwenye mitandao kwani suala la amani na Umoja na halina mbadala.

"Hatuna sababu ya kuandamana, maandamano hayana afya kwa Taifa hatuna sababu za kuharibu mali za watu binafsi hili haina afya kwa maendeleo yetu tutulie tuilinde amami yetu,"alisema.

Ndemanga aliwataka Madiwani kushirikiana na watumishi wa Halmashauri hiyo kufanikisha malengo ya kuleta maendeleo katika na kuinua mapato.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze  Leon Mgweno alisema wanatarajia kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo kutoka shule. 22 Bilion ya mwaka wa fedha 2025/2026 hadi sh.30 Bilion kwa mwaka 2026/2027.

Alisema kukua kwa mapato kwenye Halmashauri hiyo kunasaidia miradi ya Maendeleo kutekelezeka kwa haraka na kuondoa vikwazo vya maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Diwani wa Bwilingu Lawrence Tsingay aliwaahidi wananchi ushirikiano kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika kata hiyo na Halmashauri.

Aliahidi kuishauri Halmashauri kuboresha viwanja vya michezo vitakabyotumika katika mashindano mbalimbali.

Tsingay pia alisema atainua michezo kwakua kata hiyo kwa kuanzisha mashindano kwenye uoandw wa mpira wa miguu na mikono na kuibua vipaji vya michezo.