ASKOFU wa Dayosisi ya Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, ameliomba Jeshi la Polisi nchini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa Rais, Wabunge na Madiwani, wasikubali kutumiwa kwa maslahi ya watu ambao hawaitakii mema nchi.
"Jeshi letu la Polisi, nawaombeni kweli, Polisi tunawaombeni sana. Tunawategemea sana katika jambo la ulinzi na usalama na wote wanaohusika.
Zaidi aliongeza, "Niwaombe katika uchaguzi huu. Kila mmoja kwa dhamiri yake aangalie hilo na usikubali utumiwe kwa maslahi ya watu ambao hawaitakii nchi hii mema. Polisi nawaomba msisahau wajibu wenu na Mungu awasaidie."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED