MBUNGE wa Kavuu, Geophrey Pinda, amemlilia Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, kutokana na ucheleweshaji ujenzi wa barabara kutoka Kibaoni- Sitalike yenye urefu wa kilomreta 70 katika Halmashauri ya Mpimbwe, Mlele mkoani hapa.
"Barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Kavuu na halmashauri nzima ya Mpimbwe kwa kuwa ni ya kimkakati kwa uchumi wa wana Mpimbwe," alisema Pinda.
Barabara hiyo inayojengwa na Kampuni ya China Railway Seventh Gruop Co Ltd ujenzi wake uliianza mwishoni mwa mwaka 2022 na kutarajiwa kukamilika mwaka huu.
Pinda ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alitembelea eneo la barabara hiyo jana ikiwa ni sehemu ya ziara ya jimboni kwake iliyolenga kufanya ukaguzi wa shughuli za maendeleo pamoja na kuwajulia hali wananchi waliopatwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, barabara hiyo ya Kibaoni- Sitalike ujenzi wake ulitakiwa uwe umefikia asilimia 50 lakini mpaka kufikia sasa unasuasua.
"Barabara hii ni muhimu sana kwa wananchi wa Kavuu na halmashauri nzima ya Mpimbwe kwa kuwa ni ya kimkakati kwa uchumi wa wana Mpimbwe," alisema Pinda.
Pinda alimwomba Waziri Bashingwa kuitupia jicho la karibu barabara hiyo kutokana na umuhimu wake, lakini pia kuwaokoa wananchi wa jimbo lake kutokana na adha wanayoipata wanapoitumia barabara hiyo.
Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi ni moja ya maeneo ya uzalishaji mazao mbalimbali ya kilimo kama vile mpunga, mahindi, ufuta na alizeti na kukamilika kwa barabara hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji mazao hayo na kuwezesha wananchi kuinuka kiuchumi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED