Watu sita wauawa kwenye shambulizi la al-Shabaab Kenya

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 03:46 PM Mar 24 2025
Wapiganaji wa  al-Shabaab.
Picha:Mtandao
Wapiganaji wa al-Shabaab.

Watu sita wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa al-Shabaab kwenye kituo cha polisi kaskazini mashariki mwa Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za Kenya, wapiganaji wenye silaha walishambulia kambi ya polisi katika Kaunti ya Garissa, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, na kusababisha vifo hivyo.

"Polisi waliwaua washambuliaji wawili katika majibizano ya risasi," imesema taarifa hiyo.

Eneo la mpakani mwa Kenya na Somalia mara nyingi hukabiliwa na mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabaab walioko nchini Somalia.

Tukio hilo limelaaniwa na wanasiasa na wanaharakati, huku baadhi yao wakikosoa hatua za vikosi vya usalama dhidi ya raia wa eneo hilo.

(Chanzo: DW)