Dk. Slaa adakwa na polisi usiku nyumbani kwake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:24 AM Jan 10 2025
Dk. Slaa adakwa na polisi usiku nyumbani kwake.
Picha: Mtandao
Dk. Slaa adakwa na polisi usiku nyumbani kwake.

JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia kwa mahojiano aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweeden, Dk Willibrod Slaa.

Slaa alikamatwa usiku wa kuamkia leo Januari 10,2025 nyumbani kwake Bweni. Mpaka sasa Jeshi hilo halijaweka wazi tuhuma zinazomkabili mwanasiasa huyo ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro,amethibitisha kukamatwa kwa Dk. Slaa na kueleza kuwa mahojiano  yamekwenda vizuri na hivi sasa wanaangalia sheria zinasemaje ili wachukue  hatua zaidi.

Hata hivyo kamanda Muliro hakuwa tayari kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili.