Tanzania mwenyeji mkutano wa 73 wa Baraza ACI

By Cynthia Mwilolezi , Nipashe
Published at 02:22 PM Jan 10 2025
news
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la viwanja vya ndege kanda ya Afrika (ACI) ambapo wataalamu wa viwanja vya ndege nchini na Africa,watanufaika na kukuza ubora wakitaaluma ili kusaidia maendeleo endelevu sekta ya anga.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema wizara yake kwa kushirikiana na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania(TAA),kuwa maandalizi ya mkutano huo unaendelea vizuri, ambapo wajumbe wasiopungua 300 kutoka ndani na nje ya Africa watahudhuria mkutano huo.

Amesema katika mkutano huo utakaoanza Aprili 24 hadi 30 mwaka huu,zaidi  ya washiriki 300 kutoka nchi 54 za Afrika na nje ya Afrika yakiwemo mashirika 59 ya kibiashara yanayoendesha viwanja vya ndege 265 watahudhuria.

Aidha kauli mbiu ya mkutano huo   ni "katika kuelekea wakati ujao bora wa kijani kutumia usafiri wa anga endelevu na utalii wa ustawi wa kiuchumi".

Pia amesema lengo la mkutano hio ni kuhakikisha kunakjwepo na urndelevu, usalama na ufanisi katika usafiri wa anga sambamba na uzingatiaji wa masuala ya kimazingira.

Tukio hilo litaangazia maendeleo endelevu katika sekta ya usafiri wa anga na kuonyesha dhamira ya Tanzania katika utunzaji wa mazingira.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo, amesema Menejimenti imejipanga kuhakikisha inaimarisha matumizi ya Tehama katika viwanja vyote vya ndege pamoja na miradi ya kibiashara ili iweze kufanyika ikiwemo hati miliki ya viwanja hivyo kupatikana.

Amesema kuwa mkutano huo ni mkubwa na mamlaka ya viwanja vya ndege ,kutokana na umuhimu huo mkutano  unafanyika jijini Arusha na  nchi itapata fursa ya kujitangaza ikiwemo vivutio vyake,ssbabu wajumbe wametengewa siku moja ya kwenda hifadhini.