Mwenyekiti CHADEMA Singida Mjini akana kumuunga mkono Lissu

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 02:10 PM Jan 10 2025

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Singida Mjini,Shwahibu Mohamed.
Picha:Mtandao
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Singida Mjini,Shwahibu Mohamed.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Singida Mjini,Shwahibu Mohamed, amesema sio kweli kwamba wajumbe 29 wa mkutano mkuu kutoka Mkoa wa Singida wanamuunga mkono mgombea uenyekiti wa chama taifa Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo amesema kikao kilichoitishwa jana na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Omari Toto na kutoa tamko kwamba wajumbe wote 29 ambao ni wajumbe watakaopiga kura  katika mkutano mkuu utaofanyika Januari 21, 2025 wanamuunga mkono Lissu  sio kweli.

"Mkutano tulioitiwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa tuliambiwa ni wa mashauriano lakini kwasababu akidi ya wajumbe haijatimia tumeshangaa Mwenyekiti anaita waandishi wa habari na kutoa tamko kwamba Chadema Mkoa wa Singida wanamuunga mkono mgombea uenyekiti Tundu Lissu," amesema.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Singida Mjini,Shwahibu Mohamed.