Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022, Anna Makinda, amesema matokeo ya sensa hiyo yameisadia serikali kudhibiti udanganyifu ambao ungeisababisha kulipa mamilioni ya fedha kwa taarifa za udanganyifu katika janga la maporomoko ya matope lililotokea mwaka jana Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara mwaka 2023.
"Kwa kutumia picha ya setilati zilisaidia kwa kuonyesha majengo yote kwa uhalisia, unaweza ukapiga Kijiji ukakichukua chote na kama isingekuwa hii sensa watu wangeipiga serikali pakubwa wangeweza kusema nilikuwa na nyumba ya mabati au ng'ombe 100 wakati mwingine inakuwa sio kweli," anasema.
Makinda ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge, anasema ubora wa sensa hiyo umethibitika na Umoja wa Mataifa (UN).
Anasema lengo la mafunzo hayo ni kuvijengea uelewa vyombo vya habari ili viweze kutekeleza majukumu yao vizuri.
Anasema mafunzo hayo ni mfululizo wa yanayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuanzia Septemba 2023.
Hadi sasa klabu zote za waandishi wa habari nchini zimepewa mafunzo hayo muhimu kwa kuvijengea uwezo vyombo vya habari katika kutafsiri, kufanya uchambuzi na namna ya matumizi ya matokeo ya sensa.
Baadhi ya mada zilizotolewa ni mifumo ya upatikanaji na usambazaji Takwimu wa NBS,takwimu za nishati,uzalishaji wa takwimu,takwimu rasmi,misingi aina na vyanzo vyake, NBS na majukum yake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED